Zürich: Uswissi kama mwenyeji wa mkutano wa kimataifa juu ya mpango wa kinyukliya wa Iran
23 Julai 2006Matangazo
Uswissi inatayarisha mkutano wa kimataifa kuuzungumzia mpango wa kinyukliya wa Iran. Iran imeiomba nchi hiyo isiofungamana na upande wowote kutumia uwezo wake. Hii ni kwa mujibu wa gazeti la Neue Züricher Zeitung. Imetajwa kwamba katika mkutano huo utakaofanywa Geneva, nchi nyingine zitashirikishwa. Nchi tano zilizo na kura za turufu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pamoja na Ujerumani zimetoa vishawishi vya kiuchumi kwa viongozi wa Iran ili nchi yao iwachane na mpango wake wa kinyukliya. ran bado haijajibu juu ya jambo hilo.