Zoezi la kuwahamisha wanajeshi wa Kongo kutoka Goma laanza
30 Aprili 2025Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu ICRC imeeleza kuwa imeandamana na misafara kadhaa kutoka Goma kuelekea mji mkuu Kinshasa, ikiwa na maafisa waliopokonywa silaha zao pamoja na familia zao kutoka moja ya kituo cha Umoja wa Mataifa.
Kwa mujibu wa vyanzo vya usalama vya DRC na Umoja wa Mataifa, zoezi hilo la uhamishaji linafanyika baada ya mazungumzo marefu kati ya wawakilishi wa Umoja wa Mataifa, serikali ya Kongo na waasi wa M23.
Soma pia: DR Kongo, M23 watoa ahadi ya pamoja kufikia mapatano
Takriban wanajeshi 1,500 wa Kongo walikuwepo kwenye vituo hivyo vya Umoja wa Mataifa kufikia mwanzoni mwa mwezi Aprili.
ICRC imesema katika taarifa kuwa, zoezi hilo litachukua siku kadhaa na kwamba pande zote zinazohusika zimetoa ahadi ya kuhakikisha usalama wa watu walioko kwenye misafara hiyo.