Ziara ya Rais Mkapa wa Tanzania nchini Ujerumani
10 Februari 2005Suali:
Mheshimiwa Rais kwanza una maoni gani juu ya hali ya uhusiano wa kiuchumi kati ya Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani na nchi yako Tanzania ?
Mkapa:
Kwanza nataka kutoa shukrani kwa niaba ya serikali yangu na wananchi wa Tanzania kwa misaada tunayopata kutoka Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani. Kwanza kwa kutufutia madeni yetu rasmi baina ya serikali na serikali. Pili kwa misaada ya moja kwa moja katika miradi mbali mbali ya maendeleo na hasa katika eneo la afya. Misaada hiyo tunaitilia vizuri kwa sababu sera zetuza maendeleo zinalenga maendeleo ya watu wote bila ubaguzi. Hatutajirishe viongozi hata kidogo.,tunawahudumia wananchi wote.
Suali:
Jee mmejiandaa namna gani kurahisisha uwekezaji wa watu kutoka Ujerumani ?
Mkapa:
Hatuna mpango maalum kwa wawekezaji kutoka Ujerumani. Lakini kwa jumla kwa wawekezaji wote kutoka nje tumeandaa mazingira ambayo wenye nia wanaweza kuwekeza kwa faida yao lakini vile vile kwa maendeleo kwa nchi yetu. Tumerahisisha taratibu za kupata leseni za kuwekeza, tumerahisisha, tumeondoa vikwazo vilivyokuwepo vya kisheria na vya utaratibu vilivyovikichelewesha sana urejeshwaji au upelekaji wa faida zinazopatikana na wawekezaji katika nchi yetu kupeleka nyumbani kwao-tumerahisisha hilo. Tumejaribu kufanya marekebisho ya mfumo wetu wa kodi kusudi usiwe na bugudha sana na wala kama vile tusivyopenda sisi tunyonywe. lakini na sisi .tusiwanyonye., Kwa hiyo kwa jumla tumeandaa mazingira ya uwekezaji ambayo yataleta faida na yanarahisisha wenya faida kuzipeleka sehemu yoyote anakotaka kuzipeleka.
Suali:
Jee ni Maeneo gani yanayohusika na uwekezaji ?
Mkapa:
Ninasikitika kwamba hatuna wawekezaji. wengi sana lakini eneo la kilimo ni mojawapo na hasa kilimo cha mazao ambayo yanaweza kutumika kama mali ghafi katika viwanda kama vile mkonge, lakini vile vile eneo jengine kubwa ambalo lina uwezekano mkubwa sana wa kukua ni eneo la utalii. Mimi ningependa kuona watalii wengi zaidi kutoka Ujerumani na kama wakitaka kuwa na uhakika kwamba watapata chakula kinachofanana na huko nyumbani au malaazi yanayofanana au huduma inayofanana na hii wanayo ijuwa huku , tunawakaribisha wawekezaji katika, tunawakaribisha..katika usafiri vile vile waweze kurahisisha wataali wengi zaidi waje katika nchi yetu. Nafasi ni kubwa, ukarimu wetu ni maarufu unajulikana dunia kote na uhakika wa usalama wa maisha lakini vile vile wa usalama wa .rasili mali zao, ninauthibitisha katika mahojino yangu nawe.