ZIARA YA KUISAIDIA IRAQ:
11 Januari 2004Matangazo
TOKYO: Waziri wa ulinzi wa Ujapani,Shigeru Ishibu ameanza ziara yake barani Ulaya kuzungumza juu ya misaada kwa ajili ya Iraq.Mwishoni mwa mwaka uliopita serikali ya Ujapani,licha ya upinzani wa wananchi,iliamua kupeleka kiasi ya wanajeshi 1,000 kusaidia kazi za ujenzi nchini Iraq.Theluthi moja ya askari hao wanatazamiwa kuwenda Iraq wiki ijayo,ikisemekana kuwa hao wanakwenda kwanza kuichunguza hali ya usalama.Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Ujapani,idadi kubwa ya wanajeshi huenda wakapelekwa Iraq kati ya Februari na Machi.Ziara ya waziri Ishiba inampeleka kwanza Uingereza,baadae zikifuata Uholanzi na Ufaransa.Anataraji kurejea Ujapani siku ya Ijumaa.