Ziara ya kiongozi wa kanisa katoliki katika jimbo alikozaliwa la kusini mwa Ujerumani
13 Septemba 2006Matangazo
Regensburg:
Kongozi wa kanisa katoliki ulimwenguni,Papa Benedikt wa 16 amekosoa japo si moja kwa moja,itikadi kali za kiislam akisema wazo la „vita vya jihad“ haliingii akilini na haliambatani na maumbile ya Mungu.Kiongozi wa kanisa katoliki ulimwenguni amesema hayo katika hotuba yake katika chuo kikuu cha Regensburg,alikowahi kusomesha fani ya tabia,na sifa za Mungu na dini katika miaka ya 70.Papa Benedikt wa 16 amejiepusha lakini na kuikosoa moja kwa moja dini ya kiislam.Kiongozi wa kanisa katoliki ulimwenguni,mzaliwa wa Ujerumani,anaendelea na ziara yake katika jimbo alikozaliwa la Bavaria.Hii leo anatazamiwa kuzuru makaburi ya wazee wake.