Ziara ya Kanzela Merkel wa Ujerumani nchini Urusi.
26 Aprili 2006Kanzela Angela Merkel wa Ujerumani akiandamana na mawaziri wake na ujumbe mkubwa wa wanaviwanda wa Ujerumani amefunga safari kuelekea chuo kikuu cha Tomsk huko Sibiria, kwa mashauriano ya kikawaida baina ya nchi hizi mbili.Akiwasili tu Kanzela Merkel atakutana kwa mazungumzo na mwenyeji wake Wladmir Putin.
Mazungumzo kati ya Kanzela Merkel wa Ujerumani na rais Putin wa Urusi hasa yatatuwama juu ya mzozo wa mradi wa kinuklia wa Iran,lakini pia mada nyengine za kimataifa zitazungumzwa.Huu ni mkutano wa kwanza baina ya viongozi hawa wawili tangu Bibi Merkel kushika wadhifa huu kutoka kwa Kanzela Schröder,rafiki wa chanda na pete wa Bw.Putin.
Mji wa Tomsk uliopo Siberia, umejiandaa vyema kumpokea Kanzela wa Ujerumani na wakaazi wa mji huo wameingiwa na shauku kubwa kujionea ghafula kuwasili kwa kundi kubwea la waandishi habari na wanasiasa .Viktor Kress,Gavana wa Tomsk,amewataka wakaazi kuonesha urafiki wao kwa wageni wao kutoka Ujerumani.Alinukuliwa kusema,
“Mkutano huu wa kilele ni upatu mzuri kupigwa kuutembeza mji wetu.”
Kanzela Merkel,hakupendelea kufikia katika qasri alikotayarishiwa na wenyeji wake kwavile, jumba hilo ni mali ya kampuni la nishati la GASPROM,mali ya serikali.
“Bibi Merkel alihiyari kufikia katika ‘Hotel Magistrat’ kama mawaziri wake ,hoteli nzuri ingawa kufikia katika qasri aliloandaliwa ingelikua bora.”
Mwenyeji wa Kanzela Merkel, rais wladmir Puti n,alikwishawasili Tomsk jana usiku.Alitumia wakati hadi kuwasili kwa mgeni wake kwa mazungumzo na magavana kutoka maeneo mbali mbali ya mkoa wa Siberia ambao wamealikwa kuja Tomsk.
Kanzela Merkel kama mwenyeji wake amekwenda na ujumbe mkubwa ukiingiza waziri wake wa mambo ya nje, fedha,uchumi na mazingira.
Jioni ya leo itaanza hasa ziara ya Kanzela wa Ujerumani kwa shughuli kadhaa alizopangiwa.Baada ya kupiga picha pamoja kwa viongozi hao wawili,kikao cha kwanza cha wajumbe wa pande hizo mbili kitafanyika katika ukumbi wa maktaba ya Chuo Kikuu cha Tomsk.Jioni kabisa hii leo, wanasiasa hao 2 watakutana na wanafunzi wa kijerumani na wa kirusi waliopewa msaada wa masomo.
Hata kesho,siasa na uchumi zitawekwa kando hadi baadae:Bibi Merkel na rais Putin wanapanga kukutana na waakilishi wa warusi wa asili ya kijerumani –kwani kiasi cha 13.000 wanaishi Tomsk.
Wajerumani wamekuwa wakiishi huko tangu mwanzoni mwa karne ya 20.Chini ya utawala wa Stalin walisafirishwa huko kwa nguvu kutoka sehemu nyengine za iliokua Soviet Union.
Adhuhuri ya kesho ,kanzela Merkel na rais Putin watakutana pamoja na wanaviwanda aliofuatana nao kanzela Merkel.Kwani ujumbe wa wanauchumi kutoka Ujerumani umejumuisha wanabanki na wanaviwanda wa sekta ya nishati-Deutsche Bank,BASF,Siemens na makampuni mengine mashuhuri ya Ujerumani.