Ziara ya Kansela wa Ujerumani katika Oman
3 Machi 2005Matangazo
Muskat.
Kansela wa Ujerumani bwana Gehard Schröder amewasili mjini Muskat kuanza ziara ya siku mbili nchini Oman ambapo anatarajiwa kufanya mazungumzo na Sultan Kabus bin Said na kukutana na viongozi wa sekta ya uchumi.
Ziara hiyo ni muhimu kwa makampuni ya Ujerumani yanayowania tenda katika ujenzi wa reli ya kilometa alfu 2 nchini Oman.
Kansela wa Ujerumani anatarajiwa kuwasili katika Umoja wa Falme za Kiarabu kesho kuendelea na ziara yake katika nchi za kiarabu.