MigogoroUlaya
Zeleskyy amshukuru Trump kwa ahadi ya msaada wa kijeshi
15 Julai 2025Matangazo
Mazungumzo ya viongozi hao wawili yalifanyika saa chache baada ya Trump kutangaza mpango wa kuipatia Ukraine silaha zaidi za kujilinda na kuionya Moscow kuwa itakabiliwa na mbinyo wa kiuchumi iwapo vita vitaendelea.
Kwenye tangazo lake lililosubiriwa kwa shauku, Trump amesema Washington itapeleka silaha za kisasa nchini Ukraine ikiwemo mifumo ya ulinzi chapa Patriot, kupitia washirika wake wa Ulaya.
Pia ametishia kwamba ataziwekea ushuru wa asilimia 100 nchi zinazofanya biashara na Urusi iwapo mkataba wa amani hautapatikana ndani ya muda wa siku 50.