Zelenskyy: Putin akitaka aje Kyiv kwa mazungumzo
6 Septemba 2025Matangazo
Zelenskyy, amemweleza Putin kuwa pendekezo la rais huyo wa Urusi kwamba wakutane mjini Moscow kwa mazungumzo haliwezekani na badala yake rais wa Ukraine amependekeza kuwa ingekuwa bora kama watakuna mjini Kiev.
Zelenskyy amesema hawezi kukanyaga Moscow wakati nchi yake inashambuliwa na Urusi na kwamba hiyo ni mbinu tu ya Putin ya kuchelewesha mazungumzo.
Rais wa Ukraine ametoa wito mara kwa mara wa kukutana na Rais wa Urusi Vladimir Putin kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya kusitisha mapigano katika vita.
Kulingana na vyanzo vya Ukraine, angalau nchi saba zimejitolea kuandaa mkutano kati ya Urusi na Ukraine ikiwa ni pamoja na Uturuki na nchi tatu za Ghuba zinazochukuliwa kuwa haziegemei upande wowote katika mzozo huo.