MigogoroUlaya
Zelenskyy ataka mbinyo kwa Urusi baada ya shambulizi la Kyiv
20 Juni 2025Matangazo
Shambulizi hilo la droni na kombora lililotokea siku ya Jumanne, linatajwa kuwa ndiyo baya zaidi nchini Ukraine tangu kuanza kwa mwaka huu. Watu 28 waliuawa na wengine 142 walijeruhiwa pale Moscow ilipolilenga jumba hilo la ghorofa na kuliporomosha.
Zelenskyy akiwa ameambatana na Waziri wa Mambo ya Ndani, Ihor Klymenko, walilitembelea eneo la mkasa huo jana Alhamisi na kuweka mashada ya maua.
Katika ujumbe wake kupitia mtandao wa Telegram kiongozi huyo wa Ukraine amesema ni sharti Urusi ilazimishwe kusitisha vita na amewashukuru washirika wa nchi yake anaosema wako tayari kuongeza mbinyo dhidi ya Moscow.