MigogoroUlaya
Zelenskyy amtaka Putin kuhudhuria mazungumzo ya Uturuki
13 Mei 2025Matangazo
Amesema lengo lake ni wafanye mazungumzo ya ana kwa ana ya kumaliza vita kati ya nchi hizo mbili vilivyopindukia miaka mitatu.
Zelenskyy amewaambia waandishi mjini Kyiv kuwa ataongoza mwenyewe ujumbe wa nchi yake kwenye mazungumzo yaliyopendekezwa na Putin nchini Uturuki na kwamba yeye na Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki watamngoja kiongozi huyo wa Urusi mjini Ankara ama Istanbul.
Amesema iwapo Putin hatoonekana kwenye mazungumzo hayo atakuwa amedhihirisha kutokuwa na dhamira ya kweli ya kumaliza vita.
Hadi sasa Putin hajathibitisha kuhudhuria mazungumzo hayo ambayo Rais wa Marekani Donald Trump amezirai pande zote mbili kushiriki kama sehemu ya jitihada za Washington za kukomesha mapigano.