Zelensky : Ulaya kufanya mengi kuhakikisha amani Ukraine
22 Februari 2025Matangazo
Katika hotuba yake iliyopeperushwa kupitia televisheni ya taifa Ijumaa baada ya kuzungumza na viongozi wa nchi za Ulaya zikiwemo Ujerumani na Poland, Zelensky alisema Ulaya lazima na inaweza kufanya mengi zaidi ili kuhakikisha kuwa amani inapatikana nchini Ukraine.
Rais Donald Trump awataka Putin na Zelensky kukutana
Zelensky ameongeza kuwa inawezekana kufikia mwisho wa vita na Urusi kwa sababu Ukraine na washirika wake wa Ulaya wana mapendekezo ya wazi.
Rais huyo ameongeza kuwa katika msingi huo, wanaweza kuhakikisha utekelezaji wa mkakati wa Ulaya, na kwamba ni muhimu utekelezwe kwa ushirikiano na Marekani.