SiasaUkraine
Zelensky: 'Mapatano' hayataifanya Russia kumaliza vita
11 Agosti 2025Matangazo
Ukraine ina hofu kuwa huenda Trump na Putin wakawa makubaliano yatakayolazimisha Ukraine kuachia maeneo yake kwa Urusi.
Zelensky amesema Urusi inaendelea kuua watu na haipaswi kupata faida yoyote huku akisisitiza kuwa mauaji hayawezi kusawazishwa na mapatano.
Mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya wanakutana kujadili mkutano huo, huku wengi wakihofia makubaliano yanaweza kufikiwa bila ushiriki wa Ukraine.
Urusi, ambayo iliivamia Ukraine mwaka 2022, imedai kukiteka kijiji cha Fedorivka mashariki mwa Donetsk, huku mashambulizi ya angani yakiongezeka pande zote.
Ukraine imedai kushambulia kiwanda cha kutengeneza sehemu za makombora nchini Urusi.