Zelensky: Maafisa wa Marekani na Ukraine kukutana Ijumaa
28 Agosti 2025Matangazo
Akilihutubia taifa kwa njia ya video Jumatano usiku, Zelensky amesema Mkuu wa Ofisi ya Rais wa Ukraine, Andriy Yermak na Katibu wa Baraza la Usalama na Ulinzi wa Taifa, Rustem Umerov, watakutana na ujumbe wa Rais Donald Trump mjini New York.
Kabla ya kwenda Marekani, ujumbe wa Ukraine utaelekea nchini Uswisi.
Zelensky amebainisha kuwa Ukraine inaandaa maeneo ambayo yatakuwa tayari kuwa mwenyeji wa mkutano wa viongozi wa Urusi na Ukraine.
Zelensky amesisitiza kuwa Urusi lazima ishinikizwe kuchukua hatua madhubuti na za kweli kuvimaliza vita.
Wakati huo huo, maafisa wa Kiev, wamesema Alhamisi kwamba takribani watu watatu wameuawa na wengine tisa wamejeruhiwa, katika mashambulizi ya anga ya Urusi kwenye mji huo.