Zelensky kukutana na JD Vance mjini Munich Ijumaa
11 Februari 2025Matangazo
Rais wa Marekani Donald Trump pia alithibitisha hapo jana kwamba hivi karibuni atamtuma mjumbe wake maalum Keith Kellogg, kwenda Ukraine, akiwa na jukumu la kuandaa pendekezo la kusitisha mapigano. Trump anashinikiza kumalizika haraka kwa mzozo huo, wakati Zelenskyanatoa wito wa hakikisho la usalama kutoka Washington kama sehemu ya makubaliano yoyote na Urusi. Kyiv inahofia kwamba suluhisho lolote lisilojumuisha ahadi za kijeshi, kama vile uanachama wa jumuiya ya NATO au kutumwa kwa wanajeshi wa kulinda amani, kutaipa muda Kremlin wa kujipanga upya kuanzisha mashambulizi.