Zelensky: Kampuni za Magharibi zasambaza vifaa kwa Urusi
21 Juni 2025Matangazo
Rais huyo wa Ukraine ameongeza kuwa makampuni kutoka Jamhuri ya Czech na Ujerumani ni miongoni mwa yale yaliyohusishwa na vitendo hivyo.
Zelenskyy ataka mbinyo kwa Urusi baada ya shambulizi la Kyiv
Wakati huo huo, Ukraine imesema imepokea miili ya wanajeshi 20 wa Urusi badala ya miili ya wanajeshi wake, wakati wa mpango wa kubadilishana miili ya wanajeshi waliouawa vitani.
Zelensky ameishtumu Urusi kwa kutothibitisha miili inayotuma na kusema huendaUrusiinafanya hivyo kwa makusudi ili kuchanganya idadi ya miili ya wanajeshi wa Ukraine walio nayo, huku akiongeza kuwa wakati mwingine miili hiyo ilikutwa na pasipoti za Urusi.
Taarifa imeeleza kuwa mwili wa mamluki wa Israel anayepigania Urusi pia ulikuwa miongoni mwa miili hiyo iliyotumwa.