Zelensky: Nchi za Magharibi zichukue "hatua za wazi"
9 Agosti 2025Matangazo
Zelensky ameyasema hayo Jumamosi alipofanya mazungumzo kwa njia ya simu na Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer. Zelensky ameitoa kauli hiyo baada ya taarifa kuthibitika kuwa Rais wa Marekani Donald Trump atakutana na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin Ijumaa ijayo huko Alaska ili kujadili namna ya kuvimaliza vita vya Ukraine.
Hata hivyo Rais Zelensky amepuuzilia mbali mkutano huo kati ya Trump na Putin , akisema makubaliano yoyote yatakayofikiwa bila kuihusisha Ukraine "yataambulia patupu". Ukraine imesema haitakubali mkataba wowote wa amani utakaoondoa uwezekano wa kurejesha maeneo yake ya ardhi iliyoyapoteza.