SiasaUkraine
Zelensky awataka washirika wake kuwekeza kwenye madini yake
8 Februari 2025Matangazo
Kauli ya rais huyo wa Ukraine inajiri baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kusema ataipatia Kiev msaada wa kijeshi kwa kubadilishana na madini hayo adimu.
Zelensky amechapisha kwenye mitandao yake ya kijamii, akisema Ukraine inazo rasilimali za madini, lakini haimaanishi kuwa watazitoa bure kwa mtu yeyote, hata kwa washirika wa kimkakati, akisisitiza kuwa wanapaswa kuwekeza kwa faida ya pande zote.
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz alikosoa kauli ya Trump pamoja na sera zake za kigeni na kusisitiza kuwa mataifa ya Ulaya yanaisaidia Ukraine bila kutarajia malipo yoyote, na kwamba huo ndio unapaswa kuwa msimamo wa kila mtu.