SiasaUkraine
Zelensky avimwagia sifa vikosi vya anga
28 Mei 2023Matangazo
Akizungumza na wanajeshi hao mapema hii leo, Zelensky amewashukuru kwa kazi waliyoifanya akisema kila wanapoangusha ndege zisizo na rubani kutoka upande wa adui, wanafanikiwa kunusuru maisha ya watu.
Kiongozi pia ametoa salamu za shukrani kwa wafanyakazi wa huduma za uokozi waliowasaidia wahanga wa uharibu uliotokea kwenye majengo baada ya kudunguliwa kwa droni za Urusi.
Kwenye shambulizi hilo ambalo Ukraine imesema ilidungua droni 40kati ya 54 zilizorushwa na Urusi, watu wawili wamepoteza maisha na wengine watatu walijeruhiwa.
Ukraine imesema hilo ni shambulizi kubwa zaidi kuwahi kufanywa na Moscow tangu ilipoivamia nchi hiyo.