Zelensky asema yuko tayari kushirikiana na Marekani
3 Machi 2025Katika ujumbe aloutuma kupitia mtandao wa Telegram, Zelensky amaesema nchi yake inahitaji amani na kumalizwa vita vinavyoendelea lakini amesisizita kwamba msimamo kuhusu njia ya kuvimaliza vita hivyo utaamuliwa kwa pamoja na washirika wake wa Ulaya.
Ujumbe wake unafuatia mkutano wa viongozi wa Ulaya uliofanyika jana mjini London, ambao uliahidi kuongezwa bajeti za ulinzi kwa mataifa ya Ulaya na kuunda kundi la nchi zitakazokuwa tayari kusimamia utekelezaji wa mkataba wa kusitisha vita nchini Ukraine.
Mkutano huo uloitishwa na Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer, ulifanyika siku mbili tu tangu Zelensky alipozozana na Rais Donald Trump wa Marekani kwenye Ikulu ya White House, tukio liliotishia kuyasambaratisha mahusiano kati ya viongozi hao wawili.