MigogoroUkraine
Zelensky: Niko tayari kukutana na Putin kwa mazungumzo
12 Mei 2025Matangazo
Zelensky ameandika katika mtandao wa kijamii wa X kuwa wanasubiri usitishaji kamili na wa kudumu wa mapigano, kuanzia leo, ili kutoa msingi unaohitajika kwa diplomasia.
Kiongozi huyo wa Ukraine ameongeza kuwa, hakuna maana yoyote ya kuendeleza mauaji.
Soma pia: Urusi yazitaka Marekani na nchi za Ulaya kuacha kuipatia Ukraine silaha
Hata hivyo hakukuwa na majibu yoyote kutoka Ikulu ya Urusi, Kremlin kuhusu utayari wa Zelensky kuzungumza na Putin.
Zelensky na viongozi wa Ulaya walichukua msimamo mwisho wa wiki kwamba hakutafanyika mazungumzo yoyote hadi Putin atakapokubali kusitisha mapigano kwa siku 30 bila masharti kuanzia leo Jumatatu, ingawa Urusi imekataa.