Zelensky: Urusi inaukwepa mkutano kati ya yangu na Putin
22 Agosti 2025Zelensky pia ametoa wito kwa washirika wa Ukraine kuiwekea Urusi vikwazo vipya kama haitoonesha dhamira ya kweli ya kusitisha uvamizi wake Ukraine.
Rais huyo wa Ukraine aliyekuwa akizungumza katika mkutano wa pamoja wa waandishi habari na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya kujihami NATO Mark Rutte mjini Kyiv, amesema walijadili hakikisho la usalama la mataifa mengine kwa taifa lake, linalopaswa kuwa sawa na kifungu cha NATO inayosema shambulizi dhidi ya nchi moja au zaidi za Ulaya litachukuliwa kama shambulizi dhidi ya wote.
Trump atangaza mazungmzo ya pamoja kati ya putin na Zelensky
"Tunahitaji kuwalazimisha kushiriki katika diplomasia, tunahitaji vikwazo vikali sana ikiwa hawatakubali suluhisho la kidiplomasia kwa vita hivi kama hawataki kusitisha vita, tunategemea sana vikwazo kutoka kwa washirika wetu kwenda kwa Urusi. Hakikisho la usalama kwa Ukraine huenda linapaswa kufanana na kifungu cha tano cha mkataba wa NATO. na hili litaleta ufanisi. Haya ndiyo matokeo tunayopaswa kufikia."
Zelenskiy amekuwa akitoa ombi la mara kwa mara la kukutana na Putin. Hivi karibuni wakati wa mkutano wa Donald Trump na viongozi wa Ulaya mjini Washington, Rais huyo wa Marekani alisema Putin aliridhia ombi hilo kupitia njia ya simu.
Hata hivyo Urusi imekanusha uwepo wa mkutano wa aina yoyote kati ya viongozi hao wawili.