Zelensky asema Urusi imefanya shambulizi mkoani Odesa
20 Agosti 2025Matangazo
Kupitia mtandao wa X, Zelensky amesema kuwa hayo yote ni mashambulizi ya kiishara ambayo yanathibitisha haja ya kuweka shinikizo dhidi ya Urusi, pamoja na kuweka vikwazo vipya na ushuru hadi diplomasia itakapofanya kazi kikamilifu.
Jeshi la Russia ladhibiti vijiji viwili katikati mwa Ukraine
Huku hayo yakijiri, takriban watu 14 ikiwa ni pamoja na familia yenye watoto watatu, walijeruhiwa katika shambulizi la usiku kucha la Urusi katika eneo la kaskazini la Sumy. Haya yamesemwa leo na waziri mkuu wa nchi hiyo Yulia Svyrydenko.
Katika ujumbe kwenye mtandao wa X, Svyrydenko amesema watoto waliojeruhiwa katika shambulizi hilo lililolenga jumba la makazi walikuwa na umri wa miezi mitano, miaka minne na sita.