MigogoroUkraine
Zelensky asema Ukraine inataka amani na Urusi
10 Machi 2025Matangazo
Zelensky anatarajiwa kuwasili Saudi Arabia hapo baadaye, siku moja kabla ya mazungumzo muhimu kati ya maafisa wa Ukraine na Marekani yanayolenga kujadili namna ya kuusuluhisha mzozo huo uliodumu kwa zaidi ya miaka mitatu.
Soma pia: Urusi yafanya mashambulizi ya makombora Ukraine
Mazungumzo hayo yanafanyika wiki kadhaa baada ya Zelensky kutibuana na rais wa Marekani Donald Trump katika ikulu ya White House na kupelekea Marekani kusitisha msaada wa kijeshi kwa Ukraine.
Hata hivyo, Ikulu ya Kremlin ya Urusi ambayo imesifu msimamo wa Washington kuhusu mzozo huo tangu Trump aingie madarakani, imesema leo kwamba Urusi haitegemei matokeo maalum au madhubuti kutoka kwa mazungumzo hayo yanayotarajiwa kufanyika Saudia.