SiasaUkraine
Zelensky asema jeshi lake linahitaji muda zaidi
11 Mei 2023Matangazo
Zelensky amesema kwenye mahojiano na shirika la habari la Uingereza, BBC mapema leo kwamba haitakuwa sawa kuanzisha mashambulizi hayo kwa sasa kwa kuwa yangeweza kusababisha vifo vya raia wengi.
Ukraine inakabiliana na uvamizi wa Urusi kwa zaidi ya miezi 14 sasa. Kulingana na BBC, rais wa Urusi, Vladimir Putin anataka kuvipunguza vita hivyo hadi kile kinachojulikana kama "mzozo ulioganda"- hali ya kukamilika kwa vita bila ya makubaliano rasmi ya amani ambapo hakutakuwa na upande unaoweza kumuondoa mwenzake, akiamini misaada mikubwa ya kijeshi kutoka magharibi itapungua siku za usoni.