Zelensky apendekeza mataifa mengine katika mazungumzo
27 Agosti 2025Matangazo
Katika hotuba yake aliyoitoa kwa njia ya vidio, Zelensky alisema mazungumzo na wawakilishi wa mataifa hayo yatafanyika baadaye wiki hii.
Rais huyo wa Ukraine pia ametoa wito wa Urusikuwekewa shinikizo zaidi la kimataifa ili kuachana na vita vyake Ukraine huku akisema ishara Moscow inayotoa ni kwamba haitaki kuingia katika mazungumzo hayo.
Zelensky atoa wito wa mkutano na Putin kutafuta amani
Urusi na Ukraine walikuwa na mazungumzo yao ya kwanza ya ana kwa ana tangu mwaka 2022 mjini Istanbul mapema mwaka huu na kufikia makubaliano machache juu ya masuala ya kibinaadamu kama ubadilishanaji wa wafungwa pamoja na wanajeshi wa pande zotewaliouwawa wakati wa vita, lakini hawakuafikiana juu ya makubaliano mapana kama usitishwaji vita kikamilifu.