Zelensky apata uungwaji mkono wa EU na NATO
11 Agosti 2025Matangazo
Viongozi wa Ulaya wanaendelea kushinikiza kushirikishwa kwa Ukraine katika mazungumzo hayo. Afisa wa Ikulu ya White House amesema Trump haoni pingamizi lolote kwa Zelensky kuhudhuria lakini maandalizi yanayoendelea ni kwa ajili ya mkutano wa nchi mbili pekee.
Hata hivyo Ukraine imesisitiza kuwa hakuna makubaliano yoyote yatakayofanikiwa bila wao kushirikishwa. Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO Mark Rutte amesema mkutano huo wa Ijumaa utakuwa kipimo cha kutathimini ni kwa kiasi gani Putin yuko tayari kukomesha vita vyake na Ukraine.