Zelensky anapanga kuhudhuria mkutano wa NATO
18 Juni 2025Matangazo
Duru katika ofisi ya rais zimesema Jumatano kuwa uamuzi utafikiwa siku moja kabla ya mkutano huo.
Kulingana na vyanzo hivyo, hiyo ni ratiba tu iliyopangwa, na kwamba mkutano huo ni fursa ya kudumisha uungwaji mkono na kuongeza juhudi za kusitisha mapigano.
Katika mkutano huo, viongozi wa NATO wanatarajiwa kukubaliana kuhusu kuongeza kwa kiasi kikubwa matumizi ya ulinzi kutokana na shinikizo la Rais wa Marekani, Donald Trump.
Wanadiplomasia na maafisa wa NATO wamesema Zelensky amealikwa kwa chakula rasmi cha jioni kwa ajili ya viongozi kilichoandaliwa na Mfalme wa Uholanzi, jioni ya Juni 24, ambapo Trump anatarajiwa kuhudhuria.
Zelensky anaweza pia kuhudhuria kongamano la sekta ya ulinzi litakalofanyika pembezoni mwa mkutano wa kilele.