Zelensky yuko Uingereza kujadili mzozo wa Urusi na Ukraine
23 Juni 2025Matangazo
Akiandika katika mtandao wake wa X, Zelensky amesema ziara yake pia itajumuisha juhudi za kuchukua kusitisha mashambulizi Ukraine.
Huku hayo yakiarifiwa, droni 352 na makombora 11 ya Urusi yaliyorushwa Ukraine yamesababisha vifo vya watu 10 mjini Kiev.
Ukraine: Urusi imetekeleza wimbi jipya la mashambulizi na kuulenga mji wa Kyiv
Timu yawaokoaji bado inaendelea na juhudi za kutafuta miili na manusura wanaoaminika kukwama chini ya vifusi vya majengo yaliyoporomoka.
Rais Zelensky ameliita shambulizi hilo kuwa moja ya mashambulizi mabaya katika vita hivyo vinavyoelekea mwaka wake wa nne.