Zelensky: Urusi kushinikizwa kufikia amani na Ukraine
23 Agosti 2025Baada ya kuzungumza na rais wa Afrika Kusini Cyril Ramapahosa Zelensky aliandika katika ukurasa wake wa X, kwamba yuko tayari kukutana na Putin lakini Urusi inajikokokota katika kufikia amani ya mgogoro wake na Ukraine.
Huku hayo yakiarifiwa Urusi imesema vikosi vyake Mashariki mwa Ukraine vimedhibiti vijiji viwili vya Sre-dneye na Kleban-Byk katika eneo la Donetsk, wakati viongozi wa dunia wakingangana kujaribu kufikia makubaliano ya kumaliza mgogoro uliopo kati ya mataifa hayo mawili hasimu.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky aiomba Jamii ya Kimataifa kuendelea kuishinikiza Urusi
Haya yanatokea huku matumaini yakififia ya kufanyika mkutano kati ya Putin na Zelensky unaoungwa mkono na rais wa Marekani Donald Trump anayepambana kupata suluhu ya mgogoro huo.