SiasaUkraine
Zelensky amelipinga pendekezo la Rais wa Urusi
4 Mei 2025Matangazo
Rais wa Ukraine ameliita pendekezo hilo kuwa ni la kujionyesha tu. Hata hivyo Zelensky amesema Ukraine ipo tayari kusimamisha mapigano kwa ukamilifu.
Urusi imesema pendekezo hilo ambalo limetolewa kwenda sambamba na maadhimisho ya ushindi wa vita vya pili vya dunia mnamo tarehe 9 Mei, linalenga kuujaribu utayarifu wa Ukraine juu ya kuleta amani ya muda mrefu.
Urusi pia imemshutumu Zelensky kwa kutoa vitisho vya moja kwa moja kuyalenga maadhimisho hayo. Viongozi kutoka nchi zaidi ya 20, ikiwa pamoja na rais Xi Jinping wa China wanatarajiwa kuhudhuria maadhimisho ya tarehe 9 yatakayofanyika kwa gwaride la kijeshi mjini Moscow.