MigogoroUkraine
Zelensky kukutana na Putin baada ya dhamana za usalama
21 Agosti 2025Matangazo
Kiongozi huyo wa Ukraine ameyataja mataifa ya Uswisi, Austria au Uturuki kama sehemu zinazofaa kuuandaa mkutano huo.
Zelensky ameeleza kuwa anahitaji ufafanuzi wa kina kuhusu mpangilio wa Ukraine kuhakikishiwa usalama wake ndani ya muda wa siku saba hadi kumi kabla ya kukutana na Putin.
Pia amependekeza mkutano huo uwe wa pande tatu, ukimuhusisha pia Rais wa Marekani, Donald Trump.