Zelensky aishutumu Urusi kwa kutaka kuendeleza vita vyake
20 Mei 2025Matangazo
Matamshi haya ameyatoa siku moja baada ya Rais wa Marekani Donald Trump, kuzungumza kwa njia ya simu na Zelensky na Rais wa Urusi, Vladmir Putin kuhusu vita hivyo.
Zelensky ameandika katika mtandao wa kijamii kwamba ni dhahiri Urusi inajaribu kupoteza muda kwa lengo la kuendeleza vita vyake na uvamizi wake.
Kulingana na Zelensky, Ukraine iko tayari kwa muundo wowote wa mazungumzo ambao utakuwa na matokeo mazuri.
Amebainisha kuwa ikiwa Urusi itaendelea kuweka mezani madai yanayokwamisha kupigwa hatua, lazima hatua kali zichukuliwe.
Rais huyo wa Ukraine amesema hali hiyo sio tu ilishindwa kufafanua mustakabali wa mazungumzo hayo, bali pia yanaifanya hali kuwa ya kukanganya.