Zelenskiy yuko tayari kubadilishana maeneo na Urusi
12 Februari 2025Matangazo
Urusi imemuachia mfungwa mmoja raia wa Marekani, katika kile ambacho Rais Donald Trump anakielezea kama nyota njema kuelekea kuvimaliza vita.
Zelensky huko nyuma alikataa kubadilisha eneo lolote baada ya Urusi kuivamia nchi yake mapema mwaka 2022.
Lakini kwenye mahojiano na gazeti la The Guardian yaliyoachapishwa jana Jumanne, Zelensky alisema yuko tayari kwa mazungumzo ya kina kabla ya Mkutano wa Usalama wa Munich utakaoanza Ijumaa, ambapo atakutana na Makamu wa Rais wa Marekani J.D Vance, anayepinga vikali msaada wa kijeshi wa Marekani nchini Ukraine.
Maeneo hayo ni yale ambayo iliyakamata katika mkoa wa Kursk nchini Urusi, ilipofanya uvamizi wa kushtukiza mwaka uliopita.