Zelenskiy awashukuru viongozi wa Ulaya kwa kumuunga mkono
10 Agosti 2025Shinikizo la kuijumuisha Ukraine linatokea kabla ya mkutano uliopangwa kati ya Rais wa Marekani Donald Trump na Rais wa Urusi Vladimir Putin.
Mkuu wa sera kigeni wa Umoja wa Ulaya, Kaja Kallas, amesema kuwa makubaliano yoyote kati ya Washington na Moscow ya kumaliza vita vya Ukraine lazima yaijumuishe Ukraine na Umoja wa Ulaya na kuongeza kuwa ataitisha mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa Ulaya siku ya Jumatatu kujadili hatua zinazofuata.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy amewashukuru viongozi wa Ulaya kwa kuunga mkono azma ya kushiriki mazungumzo ya amani, wakati Urusi na Marekani zikijiandaa kwa mkutano wiki hii ambao Kyiv ina hofu unaweza kujaribu kuiwekea masharti magumu ya kumaliza vita vya miaka 3 na nusu.
Rais wa Marekani Donald Trump anapanga kukutana na Rais wa Urusi Vladimir Putin huko Alaska siku ya Ijumaa.