Zelenskiy: Ukraine kushinda vita ni sharti iishambulie Urusi
22 Agosti 2025Matangazo
Akizungumza wakati wa hotuba yake ya video ya kila jioni kupitia mtandao wa Telegram, Zelenskiy amesema Rais Vladimir Putin wa Urusi haelewi chochote isipokuwa mamlaka na shinikizo.
Matamshi haya ya Zelenskiy yanakuja baada ya Rais wa Marekani Donald Trump ambaye amekuwa akitafuta suluhu la kuufikisha mwisho mzozo huo, aliandika kwenye mtandao wake wa kijamii wa Truth Social kuwa "ni vigumu kushinda vita iwapo hautoivamia nchi ya yule aliyekuvamia."
Ukraine ilifanya mashambulizi ya kushtukiza katika eneo la Kursk mwaka jana, ila uvamizi huo haukudumu kutokana na mifumo mizuri ya kujilinda ya Urusi.