Zelenskiy akatisha ziara ya Afrika Kusini
24 Aprili 2025Matangazo
Katika ujumbe alioutoa kupitia mtandao wa kijamii wa Telegram, Zelenskiy amesema atarudi Kyiv baada ya kukutana na mwenyeji wake Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa.
Rais huyo wa Ukraine alikuwa anatazamia kupata uungwaji mkono wa Afrika Kusini katika juhudi zake za kuvimaliza vita vinavyoendelea nchini mwake na Urusi ambavyo viko katika mwaka wake wa nne sasa.
Shambulizi hilo la Urusi limefanyika baada ya mazungumzo ya amani kuonekana kugonga mwamba, huku Rais wa Marekani Donald Trump akimshambulia Zelenskiy kwa kusema anarefusha mapigano kwa kutokubali kuiachia Urusi eneo la Crimea kama sehemu ya mpango wa amani unaotarajiwa.
Trump amesema imekuwa vigumu kushirikiana na Zelenskiy ikilinganishwa na Urusi.