Zanzibar inasifika kwa uwepo wa mashamba ya viungo ambapo wageni hujifunza kuhusu karafuu, mdalasini, vanila na viungo vyingine vinavyokifanya kisiwa hicho kuwa kitovu cha biashara ya viungo kimataifa. Viungo hivyo hutumika katika tiba, mapishi na ni mojawapo ya utamaduni wa jadi visiwani Zanzibar. Makala ya Utamaduni na Sanaa inamulika jumba la makumbusho la viungo visiwani humo.