Watu laki moja watoroka mpakani Thailand na Cambodia
25 Julai 2025Matangazo
Haya yanafanyika wakati nchi hizo mbili zikiwa zinapambana katika makabiliano mabaya zaidi ya kijeshi kuwahi kutokea baina yao katika kipindi cha mwongo mmoja.
Wizara ya usalama wa ndani ya Thailand imesema zaidi ya watu laki moja kutoka mikoa minne, wamehamishwa katika makao huku wizara ya afya ikitangaza kuwa idadi ya waliofariki dunia imeongezeka na kufikia watu 14.
Awali Thailand ilitumia ndege ya kivita ya F-16 kushambulia kwa mabomu maeneo iliyoyalenga nchini Cambodia.
Nchi zote mbili zimelaumiana kwa makabiliano ya silaha ndogo ndogo yaliyotokea katika eneo linalozozaniwa, ambayo kwa haraka yaligeuka na kuwa mashambulizi ya silaha nzito.